Luke 15:1-6

Mfano Wa Kondoo Aliyepotea

(Mathayo 18:12-14)

1 aBasi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Isa. 2 bLakini Mafarisayo na walimu wa sheria wakanung’unika wakisema, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao.”

3 cNdipo Isa akawaambia mfano huu: 4 d“Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja, naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate? 5Naye akishampata, humbeba mabegani mwake kwa furaha 6 ena kwenda nyumbani. Kisha huwaita rafiki zake na majirani, na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’
Copyright information for SwhKC